Sunday 6 August 2017

Watendaji wa Mitaa - Dar es salaam

Mwananchi 4/8/2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kupitia kibali chenye Kumb:Na. FA.170/374/01/30 cha tarehe
19 Julai, 2017 kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora anapenda kuwatangazia Wananchi wote wenye sifa kuomba nafasi za kazi kama ifuatavyo:-
·         Mtendaji Wa Mtaa Daraja La III – NAFASI 38
SIFA
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha IV au VI aliyehitimu mafunzo ya Astashahada (CERTIFICATE) katika moja ya fani zifuatazo:- Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Oodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU
i. Katibu wa Kamati ya Mtaa.
ii. Mtendaji Mkuu wa Mtaa.
iii. Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa
iv. Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa.
v. Msimamizi wa Utekelezeji wa Sheria Ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Mtaa.
vi. Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama.
vii. Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umaskini katika Mtaa.
viii. Kusimamia ukusanyaji We mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote
ix. Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa, na Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
NGAZI VA MSHAHARA – TGS. B

MASHARTI VA JUMLA:
• Mwombaji lazima awe Raia wa Tanzania
• Awe amehitimu na Kupata Cheti cha Taaluma cha Kidato cha Nne (IV)
• NB. Results Slip hazikubaliki
• Awe na Cheti cha Kuzaliwa
• Barua zote ziambatanishwe na nyaraka zifuatazo:-
i) Nakala za Vyeti vya Mwombaji vilivyothibitishwa
ii) Maelezo binafsi ya Mwombaji (Curriculum Vitae)
iii) Picha ndogo za rangi (Coloured Passport size) mbili (2) za Mwombaji za hivi karibuni.
• Kila mwombaji lazima awe na Umri kati ya miaka 18 – 45
• Waombaji wenye Sifa Pungufu au zaidi na zilizotajwa hapo juu hawashauriwi kuomba kwani maombi yao hayatafanyiwa kazi.
• Barua ambazo hazikuambatishwa na nyaraka zilizotajwa hapo juu (i – iii) hazitashughulikiwa.
Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono, zikiwa na anwani kamili
Mwombaji, pamoja na namba ya simu na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

MKURUGENZI WA MANISPAA
MANISPAA VA UBUNGO
S. L. P. 55068
DAR ES SALAAM.
TAREHE VA MWISHO VA KUPOKEA MAOMBI:
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 18/08/2017, Ijumaa saa 9.30 Alasiri


No comments:

Post a Comment